Wafuasi wa Morsi wakabiliana na polisi Misri
Vikosi vya usalama nchini Misri
vimeimarisha ulinzi katika sehemu kadhaa mjini Cairo baada ya vurugu
kuzuka kutokana na makabiliano kati ya wafuasi wa Mohammed Morsi na
vikosi vya usalama katika mji huo na ule wa Alexandria.
Mwandishi wa BBC mjini Cairo Quentin
Sommerville anasema kuwa milipuko na milio mikuwa ya risasi imesikika
katika sehemu za katikati mwa mji mkuu.
Sehemu ambazo zimezingirwa ni kama
vile ambako wafuasi wa rais aliepindiliwa Mohammed Morsi waliwahi kupiga
kambi baada ya Morsi kuondolewa kwa nguvu mamlakani na vikosi vya
usalama mwezi Agosti katika operesheni iliyosababisha mamia kadhaa
kupoteza maisha.(P.T)
Pia usalama umeimarishwa karibu na
medani ya Tahrir ambako waandamanaji waliokuwa wanapinga Morsi
walikusanyika katika maandamano ya kumtaka ajiuzulu kabla ya majeshi
kumtoa madarani miezi mitatu iliopita.
Vyombo vya habari vimeripoti kutokea ghasia zaidi katika mkoa wa Kaskazini wa Sharqiya, Mashariki mwa Giza, pamoja na Kaskazini mwa mji wa bandarini wa Alexandria.
Mamia ya watu wameuwa tangu jeshi kumuondoa mamlakani Morsi mwezi Julai.
Maelfu ya wanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood pia wamezuiliwa katika miezi miwili iliopita.
Baadhi ya maafisa wakuu wa chama hicho akiwemo bwana Morsi na generali Mohammed Badie, wanazuiliwa kwa madai ya kuchochea ghasia na mauaji.
Vuguvugu hilo limelalamika na kusema kuwa maafisa wanazifanya juhudi zao dhidi yaokuonekana kama vita dhidi ya ugaidi

No comments:
Post a Comment