Taarifa za Snowden zawasaidia magaidi, zawadhoofisha majasusi

Ofisa wa kitengo cha Ulinzi na Usalama
cha Shirika la Ujasusi la nchini Uingereza, MI5 ameonya kuwa taarifa za
siri zilizowekwa hadharani na Edward Snowden hasa kuhusu nchi hiyo
kuhusika na kusikiliza mawasiliano ya watu, huenda zikawa zawadi nzuri
kwa magaidi kwani hatua ya kuanika upenuni mbinu hizo zimesababisha
magaidi wajichunge zaidi na hivyo kudhoofisha nguvu ya majasusi ya
kutambua mipango ya magaidi na kuyashughulikia kabla ya hatari.(P.T)
Kwa mujibu wa shirika la habari la
Reuters, Mkurugenzi wa MI5, Andrew Parker alikiri kuwa wafanyakazi wa
vitengo vya ulinzi na usalama vya nchi za Marekani na Uingereza
vilitegemea sana mawasiliano ya magaidi ili kutengua mitego kabla ya
hatari lakini kwa sasa, kitengo chao cha kusikiliza mawasiliano, GCHQ,
kimepata pigo kubwa kwa kuwa sasa magaidi wanatumia mbinu nyingine ili
kufanikisha mashambulizi waliyopanga.
Source: http://www.wavuti.com
Source: http://www.wavuti.com
No comments:
Post a Comment