MUSEVENI,Dk BESIGYE WAKUTANA ANA KWA ANA
Wapinzani wawili wa kisiasa, Rais
Yoweri Museveni na mpinzani wake mkuu, Dk Kizza Besigye wamekutana ana
kwa ana kwenye sherehe za Uhuru huko Rukungiri, siku moja baada ya Rais
Museveni kumrushia vijembe Besigye.
Wawili hao wanakutana baada ya Museveni kumtaka Besigye na Meya wa Jiji la Kampala, Erias Lukwago kuacha kuchochea machafuko kwenye mji huo kwa nia ya kutaka kuiingiza nchi hiyo kwenye vurugu kama ilivyo Misri kwa sasa.(P.T)

Pia aliwataka kuacha kuingia katika
mapambano ambayo hayana faida kwao kwa kuwa mara zote wamekuwa
wakishindwa hivyo ni vyema wakirejea kwenye chama tawala, ambako
watapokelewa kwa heshima.
Maoni hayo yaliibua mvutano wa maeneo kutoka kwa Dk Besigye ambaye amewahi kuwa daktari wa Museveni ambapo alikaririwa na gazeti la Daily Monitor akihoji "Niombe samahani kwa lipi? Yeye amejifanya kuwa jaji na hilo ndilo tunapambania," alisema.
Katika maadhimisho ya leo, dhima kuu ni 'Kuimarisha fursa za uwekezaji' ambapo Rais Museveni ndiye mgeni rasmi na Dk Besigye akihudhuria kwa mwaliko rasmi wa Ikulu.

No comments:
Post a Comment