SERIKALI YA ITALIA YASHINDA KURA YA IMANI
Waziri mkuu wa Italia Enrico Letta
amepata ushindi katika kura ya imani kwa serikali yake, baada ya waziri
mkuu wa zamani Silvio Berlusconi kubadilisha mipango yake ya kuuangusha
muungano unaotawala nchini humo.
Letta amepata kura 235 katika baraza
la juu ya bunge la Italia- Seneti, ambako alikuwa katika hatari ya
kukosa wingi unaohitajika wa kura 161 kwa kura 20, iwapo mpango wa
Berlusconi kujiengua ungetimia. Maseneta 70 walipiga kura ya kumpinga.
Akizungumza katika bunge hilo lililojaa hamasa, Berlusconi alisema
wameamua bila kinyongo kupiga kura ya kuwa na imani na serikali.
Akifafanua uamuzi wake, Berlusconi alisema Italia inahitaji serikali
ambayo inaweza kufanya mageuzi ya kimuundo na kitaasisi, ambayo nchi
hiyo inayahitaji ili kuwa ya kisasa.(P.T)
Luigi Zanda, ambaye alizungumza kwa
niaba ya chama cha siasa za wastani za mrengo wa shoto cha Demokratik,
PD alisema waziri mkuu huyo wa zamani alikuwa anajaribu kuficha pigo la
kisiasa, ambalo hata hivyo liko wazi machoni mwa Wataliana. Kabla ya
hotuba ya Berlusconi, kulikuwepo na taarifa kuwa 25 kati ya wabunge 91
kutoka chama chake cha kihafidhina cha People of Freedom PDL walikuwa
tayari kupiga kura ya kuwa na imani na serikali.
Ufa katika chama cha Berlusconi
Chama cha PDL kiliendelea kuparaganyika licha ya kubadilisha msimamo katika dakika za mwisho wakati Francesco Nitto Palma, waziri wa zamani wa Sheria, alipotoka nje kuepuka kumuunga mkono Letta, na kufuatiwa na maseneta wengine wa chama hicho. Maseneta walioasi msimamo wa chama chao cha PDL waliongozwa na naibu kiongozi wa chama hicho ambaye pia ni naibu waziri mkuu Angelino Alfano, na waziri wa miundombinu Maurizio Lupi, ambaye anahusiana na vuguvugu la kihafidhina la kikatoliki lenye ushawishi mkubwa la Communion and Liberation.
Maafisa wa chama kinachoongoza muungano huo cha PD walisisitiza kuwa serikali haitaendelea kutegemea uungwaji mkono usioaminika wa waziri mkuu huyo wa zamani. Stefano Fassina, waziri mdogo kutoka chama cha PD, alisema Silvio Berlusconi ameshindwa vibaya, na kuanzia leo, hana umuhimu wowote wa kisiasa.
Masoko yanemeeka
Masoko ya hisa ya Italia yamepokea vyema matokeo ya kura hii, ambapo faharasi kuu katika soko la hisa la Milani, ilipanda kwa asilimia 0.65 kufikia saa tisa alasiri, wakati kiashirio muhimu cha hatari kilikuwa chini. Katika hotuba yake kabla ya kura hiyo, waziri mkuu Letta alisisitiza kuwa nchi hiyo inahitaji utulivu wa kisiasa ili kutoka katika mdororo wa muda mrefu wa kiuchumi na kuendeleza imani ya masoko.
Waziri mkuu huyo alisema anataka aendelee kuiongoza Italia hadi angalau mwishoni mwa mwaka ujao wa 2014, wakati Italia itakapokamilisha kipindi chake cha miezi sita ya urais wa mzunguko wa Umoja wa Ulaya. Berluscon alisema wiki iliyopita kuwa anajiondoa katika muungano wa serikali, baada washirika kukataa kuzuwia mchakato wa kumfukuza bungeni kutokana na kutiwa hatiani kwa kosa la kukwepa kodi. Atatumikia kifungo cha mwaka mmoja nyumbani au kufanya kazi za kijamii.
Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/dpae,afpe, ape

No comments:
Post a Comment