NDEGE YA ABIRIA YAANGUKA NIGERIA
Ndege iliyokuwa imewabeba watu 27
imeanguka baada ya kukumbwa na hitilafu ya injini, muda mfupi baada ya
kuruka kutoka uwanja wa ndege mjini Lagos.
Duru zinasema kuwa watu 5 wamefariki
huku shughuli ya uokozi ikendelea na mtu mmoja akipata matibabu kwa
majeraha mabaya aliyopata.
Ndege hiyo ya shirika la ndege la
Associated Airlines, iliyokuwa na uwezo wa kubeba watu 30 ilianguka muda
mfupi tu baada ya kuruka na kulipuka.(P.T)
Aidha ilikua inaelekea mjini Akure
Kusini Magharibi mwa nchi, kwa mujibu wa msemaji wa shirika la udhibiti
wa safari za angani nchini humo.
Injini ya ndege ilikumbwa na hitilafu na kuisababisha ndege kuanguka na kuteketea.
Hata hivyo hakuna taarifa za kuthibitisha idadi ya watu waliofariki.
Ndega hiyo iliruka mwendo wa saa mbili unusu kutoka katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Murtala Mohammed
Maafisa walisema kuwa ndege hiyo ilianguka karibu na bomba la mafuta katika uwanja huo.
Haijulikani ikiwa mafuta hayo ndiyo yalisababisha ndege kulipuka.
Shahidi mmoja alimbia BBC kuwa alisikia mlipuko mkubwa uliofatiwa na moshi mkubwa ukifuka kutoka katika sehemu ya ajali hiyo.
Maafisa wa usalama waliharakisha kwenda katika eneo la ajali na kuanza kuwaokoa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

No comments:
Post a Comment