KOMBE LA DUNIA 2014: UJENZI WA MOJA YA VIWANJA WAPIGWA STOP NA MAHAKAMA

Kazi ya ujenzi katika Uwanja
utakaochezewa mechi za kombe la dunia la soka mwaka 2014 nchini Brazil
zimesimamishwa baada ya jaji wa mahakama kusema kuna wasiwasi kuhusu
usalama. (HM)
Uwanja huo wa Arena da Baixada katika
jiji la Curitiba ulipangiwa kuchezwa mechi nne za kombe la dunia.
Ukarabati wa uwanja huo ulikwishacheleweshwa kwa kipindi kadhaa.
Aliamrisha ukaguzi mpya ufanywe kabla
ya kuanza tena shughuli za ujenzi. Akiongeza kusema kumegunduliwa kasoro
nyingi katika ujenzi huo.Jaji Lorena Colnago alisema maisha ya
wafanyikazi yanahatarishwa kutokana na hali ya kuzorota kwa ujenzi huo.
Akiongeza kusema kuna hatari ya kuzikwa,kukanyagwa na magari na hata
kudondoka kutoka kuta za juu za uwanja huo.
Taarifa hizo zinakuja wiki moja tu
baada ya uchunguzi kufichua kwamba wafanyikazi walioajiriwa katika
ujenzi wa mradi mwingine wa kombe la dunia walikabiliwa na hali ya
kitumwa.
Wachunguzi hao walisema pia kwamba
zaidi ya wafanyikazi 100 walioajiriwa katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Sao Paulo wanaishi katika hali duni karibu na uwanja huo.
Mnamo mwezi wa Agosti, waziri wa
michezo Aldo Rebelo alisema ana wasiwasi jinsi ujenzi ulivyochelewa
katika viwanja vitano vya michuano ya kombe la dunia mwakani.
Baada ya ziara yake nchini Brazil,
katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke,alisema viwanja vyote lazima viwe
tayari ifikapo mwezi Desemba na kuonya hatavumilia tena kuchelewesha
ujenzi na hakuna 'mpango mbadala'.
Michuano ya kombe la dunia imepangwa katika viwanja 12 nchini kote Brazil. Chanzo: shaffihdaud
No comments:
Post a Comment