Hali ya usalama ni shwari Iringa, tayari kwa nyerere day kitaifa

HALI ya usalama kwa mkoa wa Iringa
hususani Manispaa ya Iringa ni salama kwa ajili ya shughuli za
kumbukumbu ya baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere na uzimaji wa Mwenge wa
uhuru Mapema wiki ijayo. (HM)
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema jeshi hilo limejiandaa vema katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao kwa wakati wote.
Alisema kuna askari wengi kwa ajili ya kuimarisha ulinzi katika maeneo yote wakiwa na vifaa maalumu vya kubaini viashirio vya uvunjifu wa amani.
Aidha aliwataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo katika kuimarisha ulinzi katika maeneo yote na kujitokeza katika shughuli hizo za kitaifa.
Aliwatahadharisha madereva wa mkoa wa Iringa na wale waingiao na kutoka kufuata sheria za barabarani kama jinsi ya kuegesha magari, kwenye alama za punda milia na mwendo kasiili kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.
"Ni vema wale madereva wahuni na vichwa maji wakaacha kuvunja sheria za barabarani kwa kuwa tumejipanga katika kukabiliana na uvunjivu wa amani" alisema Kamanda Mungi
Aliongeza kuwa wana vifaa vya kutosha vya kuwatambua wanaovunja sheria za barabarani ikiwemo wale wanaozidisha mwendo kwa mkoa mzima. Chanzo: Hakimu Mwafongo
No comments:
Post a Comment