TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, October 9, 2013

BRAC TANZANIA KUNUFAISHA WATU LAKI MOJA

BRAC logo1 40beb
ZAIDI ya watu 100,000 watanufaika na mradi shirikishi wa kilimo cha mahindi, mbogamboga na ufugaji wa kuku wa kienyeji (LEAD) chini shirika la Brac Maendeleo katika mikoa 15 nchini. (HM)

Akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa mradi huo kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Mratibu wa LEAD, Mahfuz Ashraf alisema lengo kuu la mradi ni kuwawezesha masikini kuondoka na na umaskini kupitia fursa zilizopo kwa uwingi nchini.
Alisema kati ya watakaonufaika asilimia 61% ni wanawake hasa wa kutoka kaatika maeneo ya vijiji ikiwa ni mkakati kabambe wa kuwakomboa kuondokana na umaskini uliokithiri kwa sasa kwa wananchi.
Ashraf alisema LEAD itasaidia kuboresha uzalishaji wa kuku wa kienyeji, uzalishaji wa mazao ya mbogamboga na mahindi pia kuboresha uzalishaji wa mbegu bora na kilimo cha kisasa na mawasiliano baina ya maafisa ugani na wakulima wadogo wadogo ili kuongeza uzalishaji kwa kutumia kilimo.
Naye Meneja wa eneo wa BRAC, Amina Katela alisema mradi wa LEAD utashughulika na maeneo makuu manne ikiwemo kuboresha mahusiano kati ya wakulima na soko kupitia vikundi vya wakulima na wasambazaji wa pembejeo.
Katela alisema kutakuwa na mashamba darasa yatakayowezesha wakulima kuona na kujifunza kwa vitendo na kuweza kutumia mbinu hizo ama kwenye vikundi au mmoja mmoja.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi alisema hiyo ni fursa nzuri kwa wakazi wa maeneo ambayo LEAD inatekelezwa kwa kuwa utatoa fursa ya ajira na uhakika wa chakula kwa wananchi. Chanzo: Hakimu Mwafongo

No comments:

Post a Comment