Zambia yaadhimisha miaka 50 ya uhuru bila uwepo wa Rais Sata.
Wananchi
wa Zambia wanasherehekea maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru siku ya leo,
huku rais wa nchi hiyo Michael Chilufya Sata akiwa nje ya nchi
anakotibiwa.
Hii ni mara ya kwanza kwa rais huyo anayefahamika kama King Cobra kutoshiriki katika maadhimisho ya kumbukumbu hiyo tangu aingie madarakani mwaka 2011.
Taarifa za kuugua kwa Sata zimekuwa
zikienea kwa kipindi kirefu ambapo kuna wakati alilazimika kuhutubia
bunge la nchi hiyo na akisisitiza kwamba hajafariki kama ambavyo ilikuwa
ikidhaniwa na watu wengi baada ya kutoonekana hadharani kwa kipindi
kirefu.
Wasi wasi juu ya afya ya rais Sata
ulitanda pale aliposhindwa kuhutubia katika kikao cha umoja wa mataifa
UN, na baada ya kurejea nchini humo alitangaza rasmi kuwa anasafiri kwa
ajili ya kwenda kutibiwa nje ya nchi japo hakuweka wazi anakwenda
kutibiwa nchi gani.
Hii ni mara ya kwanza kwa rais huyo kukosekana katika maadhimisho ya siku ya uhuru tangu aingie madarakani mwezi Septemba 2011.
Mataifa mbali mbali pamoja na Marekani,
Uingereza na Ufaransa wameipongeza Zambia kwa kudumisha amani na
demokrasia huku wakiahidi kuendeleza ushirikiano uliodumu baina ya
mataifa hayo kwa kipindi chote cha miaka 50 tangu nchi hiyo ipate uhuru.
No comments:
Post a Comment