Obama apingana na unyanyapaa wa magavana wa New York, New Jersey
Rais Obama amekosoa baadhi ya sheria zilizowekwa na majimbo na nchi mbalimbali katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.
Obama amekosoa kuhusiana na sheria ya
kuweka karantini siku 21 manesi na madaktari waliotoka nchi za Afrika
Magharibi kuhudumia wagonjwa wa Ebola kwa kusema kuwa sheria hiyo
inawavunja moyo watu hao walioamua kujitolea maisha yao kwa kuwasaidia
waathirika wa ugonjwa huo.
Rais huyo hakutaja majina ya majimbo
wala nchi ambazo anazikosoa kwa sheria hizo kandamizi, lakini New York
na New Jersey zilitangaza utaratibu huo ambao ulianza kutekelezwa mwanzo
wa wiki hii hivyo inaonekana ujumbe wa Obama umelenga magavana wa
majimbo hayo.
Kauli ya Obama huenda ikawa na tafsiri
inayokosoa vilevile uamuzi uliofanywa na serikali ya Australia wa kuzuia
kuingia nchini humo mtu yoyote anayetokea ukanda wa nchi za Afrika
Magharibi ambazo zimeathiriwa zaidi na janga la ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment