Bunge lachomwa moto pamoja na nyumba za wabunge, rais agoma kuachia madaraka
Mbali na maafa makubwa yaliyojitokeza ikiwa ni pamoja na majengo ya bunge kuchomwa moto pamoja na nyumba za wabunge, rais aliye madarakani amegoma kuachia madaraka yake.
Blaise Compaore rais wa Burkina Faso
aliyekaa madarakani kwa miaka 27 anatajwa kuwa mmoja wa marais waliokaa
madarakani kwa kipindi kirefu zaidi na bado anasisitiza kuwa ana miezi
12 zaidi ya kuendelea kuwepo madarakani kabla ya kukabidhi madaraka kwa
rais ajaye.
Ban Ki-moon anatarajiwa kuwasili nchini siku ya leo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya machafuko hayo.
Chanzo cha machafuko hayo kinatajwa kuwa
ni kitendo cha bunge kutaka kufanya mabadiliko ya katiba ambayo
yangemfanya Blaise Compaore kubakia madarakani kwa kipindi kingine
zaidi.
Taarifa zinasema jeshi limelazimika kuongoza nchi hiyo ili kurejesha utulivu.
No comments:
Post a Comment