Kivumbi cha Ligi kuu England

Golikipa Simon Mignolet wa timu ya Liverpool ashindwa kuupangua mpira.
Kitimtim 
cha ligi kuu ya England kitaendelea tena kesho wakati ambapo mashabiki 
wa soka nchini humo na duniani kote watapata nafasi ya kuzishuhudia timu
 zao zikitafuta pointi tatu muhimu.
Newcastle
 Utd wataikaribisha Liverpool katika mchezo ambao utarushwa moja kwa 
moja kupitia idhaa ya Kiswahili ya BBC majira ya saa tisa unusu kwa saa 
za Afrika Mashariki.
Arsenal 
wao wataikaribisha Burnley, huku Chelsea nayo wakiialika QPR. Everton 
watakuwa nyumbani kucheza Swansea City. Hull City wataikabili 
Southampton. Michezo mingine ni itakayochezwa siku hiyo ya kesho ni kati
 ya Leicester City watakapo kwaana na West Brom, Huku Stoke City 
watakapoikabili West Ham utd.BBC
Siku ya 
jumapili ni mpambano wa kukata na shoka ambapo Manchester United 
wataavaana na Manchester City mechi ambayo pia itatangazwa moja kwa moja
 na Idhaa ya Kiswahili ya BBC ,huku Tottenham watakapokwaana na Aston 
villa.
No comments:
Post a Comment