Unafahamu kuna watu watatu waliotokea Liberia hawajulikani walipo? Isome taarifa hii
Wakenya tisa kati ya kumi na mbili waliokua wamekwama nchini Liberia tangu kulipuka kwa ugonjwa wa Ebola wamewasili usiku katika uwanja wa Jomo Kenyatta International Airport (JKIA) Nairobi, Kenya.
“..Awali tulikua tunatarajia wakenya 150
kutoka Liberia lakini ni kumi na mbili pekee walioonesha dharura ya
kusafiri kurudi nyumbani, na kama mnavyojionea tumewapokea tisa pekee na
hatufahamu wengine watatu waliko..”– Waziri Macharia.
Katika idadi hiyo ya watu tisa ni pamoja
na watoto wanne na watu wazima watano ambao walikuwa kwenye ndege
iliyotokea Brussels na abiria wengine 69 na majira ya saa 5:30 usiku wa
jana.
Kuhusiana na Wakenya wengine watatu kati ya kumi na mbili waliotarajiwa kuwasili siku ya jana bado haijafahamika wapi walipo.
Waziri amesema serikali ina mpango wa
kuwasafirisha kuwarudisha nchini humo Wakenya wengine watano kutoka
Sierra Leone hivi karibuni.
Waziri ametangaza rasmi kuwa iwapo kuna
mtu yoyote atabainika kuwa na dalili za Ebola atawekwa karantini kwa
siku 21 na wale wasio na dalili zozote wataruhusiwa kurejea majumbani
mwao.
No comments:
Post a Comment