Hawa ndio mastaa wanaogombea Ubunge jimbo moja kupitia vyama tofauti
Taarifa
 kuhusiana na mastaa mbali mbali ikiwemo wa muziki, filamu, na michezo 
kuingia katika headline zinazowangumzia kujihusisha na siasa sio taarifa
 ngeni kuzisikia, ambapo kwa sasa mastaa wa movie wanaingia kwenye 
headline nyingine ya wao kwa wao kugombea nafasi ya ubunge kwenye jimbo 
moja kupitia vyama tofauti.
Mastaa wa filamu kutoka Nigeria Bob 
Manuel Udokwu na Tony One Week Muonago wanaendelea kuzungumziwa sio kwa 
sababu wamejiingiza kwenye siasa, bali kinachozungumziwa ni kitendo cha 
wao kugombea nafasi hiyo katika jimbo moja kitu  ambacho kimeanza 
kuvutia hisia za watu wengi.

Bob Manuel Udokwu (kushoto) na Tony One Week, waigizaji wa Nollywood waliojitosa kugombea katika Jimbo la Anambra.
Bob Manuel Udokwu anagombea kupitia 
chama cha APGA na Tony One Week Muonagor anagombea kwa tiketi ya ACN 
katika jimbo moja la Anambra, Nigeria ambapo uchaguzi mkuu wa nchi hiyo 
unatarajiwa kufanyika katikati ya mwaka 2015, ambapo staa mwingine wa 
Nollywood ambaye alitangaza kujiingiza kugombea ubunge ni Desmond 
Elliot.

No comments:
Post a Comment