TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, October 7, 2014

Wiki mbili kabla ya kukutana na Yanga – Okwi apata majeruhi, Daktari azungumza

IMG_7819.JPG
Zikiwa zimebaki takribani mbili kabla ya mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga, daktari wa Simba SC, Yassin Gembe amesema kwamba mshambuliaji, Mganda Emmanuel Okwi aligongwa kwenye enka na goti katika mchezo dhidi ya Stand United, lakini yuko fiti kabisa kucheza Oktoba 18, dhidi ya Yanga SC.
Okwi alitolewa nje mara mbili kupatiwa huduma ya kwanza na Dk Gembe, lakini mara zote alirejea uwanjani kuendelea na mchezo.
Pigo la pili lilimfanya mchezaji huyo aendelee kucheza huku akichechemea, hali ambayo ilizua hofu labda amepata maumivu makubwa.
“Ni kweli Okwi aligongwa mara mbili,
mara moja kwenye enka na mara moja
kwenye goti. Lakini hayakuwa maumivu makubwa na ataendelea na mazoezi na wenzake” amesema Gembe
Aidha, Dk Gembe amesema kwamba
kipa Ivo Mapunda na beki Nassor
Masoud ‘Chollo’ wataanza mazoezi ya
kujiweka fiti wiki hii.
Ivo aliumia kidole na anatakiwa kuwa
nje kwa wiki nane, hivi sasa akiwa
yupo katika wiki ya tatu, wakati Chollo
aliyeumia mkono, anatakiwa kuwa nje
kwa wiki tatu, hivi sasa akiwa
anaingia katika wiki ya pili.
“Hawa wachezaji maumivu yao
hayawazuii kufanya mazoezi ya
kujiweka fiti, kwa hivyo niliwapa
mapumziko mafupi kabla ya kuanza
mazoezi ya kukimbia na gym. Ivo
nilimpa wiki mbili za kupumzika na
Chollo wiki moja, kwa hivyo wote wiki
hii wataanza mazoezi,” Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ na Haroun
Chanongo ambao wiki iliyopita
walifanya mazoezi mepesi, nao
wataanza mazoezi kikamilifu na
wenzao.
Majeruhi mwingine wa muda mrefu
Simba SC ni Mkenya, Paul Kiongera
ambaye anatakiwa kuwa nje kwa wiki
sita baada ya kuumia goti, hivi sasa
akiwa katika wiki ya nne- na Dk
Gembe amesema ‘fowadi’ huyo
anaendelea vizuri.

No comments:

Post a Comment