LORRAINE ATUA NCHINI APONGEZA WATANZANIA
Lorraine 
Clement akipungia watu waliofika kumlaki , alipokuwa akiwasili uwanja wa
 ndege JNI, alipokuwa akitokea nchini, Thailand, kushiriki mashindano ya
 Miss Grand International 2014, ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20 
bora.
Lorraine 
Clement akishukuru Mungu, alipokuwa akiwasili uwanja wa ndege JNI, 
alipokuwa akitokea nchini, Thailand, kushiriki mashindano ya Miss Grand 
International 2014, ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20 bora.(Martha Ma
Kwa upande wake, Mama Mzazi wa Lorraine, Paula David aliwashukuru watanzania kwa kumpigia kura mwanae na kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Hii ni kwa mara kwanza, mtanzania huyo anashiriki shindano hilo ambalo kwa hapa nchini linaendeshwa na kampuni ya Redline Communication Ltd, ambapo mshiriki wake huitwa 'Miss Grand Tanzania', kwa mwaka huu, Lorraine alikuwa ni mshindi wa pili kwenye shindano la Tanzania Top Models 2013.
Aidha, Katika shindano hilo, mwanadada, Daryanne Lees kutoka nchi ya Cuba, ndiye aliyetwaa taji hilo kwa mwaka huu. Wengine ni Miss Ethiopia, Hiwot Mamo na Miss Canada, Kathryn Kohut.
Shindano hilo la Miss Grand International, kwa sasa ni msimu wa pili likifanyika nchini Thailand, tokea kuanzisha mwaka 2013. Mshindi wa mwaka huu, ameweza kunyakua kitita taslimu cha dola za kimarekani 40,000, pamoja na thamani za ndani.
Lorraine akilakiwa na meneja wake Abubakar Faraji.
Lorrainea kiwa na familia yake na mama yake (kulia).
Na Andrerw Chale
MWANADADA
 Lorraine Clement aliyeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo 
ya kimataifa ya Miss Grand International 2014, na kufanikiwa kushika 
nafasi ya 20 bora katika shindano lililofanyika mjini, Bangkok, 
Thailand, ametua nchini jana Oktoba 9 majira ya saa 10 jioni na 
kuwashukuru watanzania kwa kumuunga mkono.
Akizungumza
 na wandishi wa habari muda mfupi alipowasili uwanja wa ndege wa 
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Lorraine 
aliwashukuru wadau mbalimbali kwa kufanikisha ushiriki wake kwenye 
mashindano hayo makubwa duniani, ikiwemo kampuni ya Redline 
Communication Ltd, Iliyofanikisha mshiriki huyo kushiriki kwa mwaka huu.
"Pongezi 
kwa wadau wote mliofanikisha mimi kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.
 Millen Magese kupitia kampuni yake ya MMG, Jacqueline Kibacha, Doreen 
Mashika, Husna Tandika na wengine weng
No comments:
Post a Comment