Canada yatoa tamko kuhusiana na shambulio la Bungeni.
Masaa
machache baada ya kutokea tukio la shambulizi la risasi katika bunge la
Canada lililopelekea mwanajeshi mmoja na askari wa bunge, kuuawa
serikali ya Canada imetoa tamko rasmi kuhusiana na tukio hilo.
Akitoa tamko hilo waziri mkuu wa Canada
Stephen Harper amesema shambulio hilo ‘haliitetemeshi’ Canada, bali
linaiongezea nchi hiyo ujasiri.
Rais wa Marekani Barack Obama na waziri
mkuu wa Uingereza David Cameron wamelaani kitendo hicho kwa kukiita ni
cha kukiita ni cha ‘kikatili’, huku wakisisitiza kuwa wakati huu ni wa
kuwa macho zaidi kwa kuimarisha ushirikiano baina yao katika kupambana
na ugaidi.
Cameron ameeleza kuwa tayari kushirikiana na Canada kwa msaada wowote utakaohitajika katika kukabiliana na hali hiyo.
Taarifa kutoka shirika la utangazaji
nchini Ufaransa RFI linasema bado askari polisi wa kikosi maalum cha
usalama wameendelea kulizunguka eneo hilo japo hali ya usalama
imeimarika kwa sasa.
Canada imesema waliouawa kutokana na
shambulio hilo ambao ni mwanajeshi koplo Nathan Cirillo na aliyekuwa
askari wa bunge Kevin Vickers wamekufa kishujaa, huku polisi wakiendelea
kumsaka mshukiwa wa tukio hilo aliyetajwa kwa jina la Michael Zehalf-
Bibeau.
No comments:
Post a Comment