KAMPENI YA HAKI YA UCHUMI KATIKA MASWALA YA KILIMO YAENDESHA MDAHALO
Meneja wa
 Kampeni haki ya Uchumi kutoka Oxfam Eluka Kibona akifungua Mdahalo huo 
na mafunzo juu ya Kujenga hoja ya upatikanaji wa Chakula na haki ya 
chakula, Kufuatilia upatikanaji wa haki kwenye Rasilimali za Ardhi na 
matumizi yake,na kuhamasisha uwekezaji kwa wakilima wadogo wadogo 
Hususani wanawake kwenye Muktadha wa mabadiliko ya Tabia nchi, katika 
kampeni ya GROW   
 Mmoja wa
 washiriki wa Semina hiyo akielezea matarajio yake akiwa kama Mama 
shujaa wa Chakula na Mkulima mwanamke Jinsi ambavyo wameweza kusaidiwa 
na Oxfam kufikia malengo yao katika kilimo na kuwa wakulima Bora wenye 
mfano wa Kuigwa
 
 Mshindi 
wa Maisha Plus 2012 Bernick Kimiro akitoa mchango wake Jinsi kilimo 
kinavyo weza kumsaidia mwanamke na kufikia Malengo yake.(P.T)
 Mshindi 
wa Mama shujaa wa Chakula 2014 , akiendelea kuchukua Maoni mbalimbali , 
Mchango na mawazo ya watu mbalimbali katika Mdahalo huo.
 Oscar Munga kutoka Forum CC akitoa ufafanuzi wa kina juu ya mahusiano ya kilimo na mabadiliko ya Tabianchi, Pia alizungumzia ni namna gani watu wanaweza kujikomboka katika kilimo na kuendana na Mabadiliko ya Tabianchi.
 Balozi 
wa Oxfam kupitia kampeni ya GROW Khadija Mwanamboka akielezea umuhimu wa
 kilimo bora na uwezeshaji wa wanawake katika kupata haki za Ardhi 
lakini pia jinsi gani Mwanamke anaweza kujikomboa katika kilimo na kuwa 
wanawake wanahaki sawa katika swala zima la kumiliki Ardhi. 
 Wa 
kwanza kulia ni mmoja wa aliyekuwa mshiriki wa Mama Shujaa wa Chakula 
2014 kutoka Zanzibar akitoa Mchango wake kuhusu Umiliki wa Ardhi na 
kuelezea jinsi gani wanawake wasivyo na haki ya Ardhi hiyo, na kuomba 
kwamba nao ni binadamu na wanahaki sawa ya kumiliki ardhi hiyo 
 Wakili 
Joseph Chiobola ambaye ni Afisa Programu kutoka Haki Ardhi akitoa 
ufafanuzi wa kina juu ya haki za watu kumiliki Ardhi, pia alieleza kwa 
kina sababu za watu mbalimbali kugombania Ardhi na kueleza namna gani 
Migogoro ya Ardhi inatokea na Njia za kuimaliza Migogoro hiyo. 
 Mkamiti Mgawe kutoka Oxfam Akichangia Jambo katika Mdahalo huo 
Afisa Ushawishi wa Ardhi kutoka Oxfam Naomi Shadrack akiendelea kutoa muongozo katika mdahalo huo.
 Mchoraji
 Maarufu wa Katuni Muhidini Msamba akitoa mchango wake juu ya mada 
ambayo ilikuwa inahusu mazao kuto kuwa na thamani kuwa ndio moja ya 
chanzo cha wakulima waliowengi kutoka Tanzania kukosa  Masoko katika 
mazao yao, aliongeza ushauri kuwa kunahitajika nguvu ya ziada ili 
kujikwamua katika swala hilo kwa ujumla 
Mama Shujaa wa Chakula 2012 akitoa ushuhuda wake jinsi Kampeni ya Grow inayoendeshwa na Oxfam Jinsi walivyo weza kumpa Shamba ambalo mpaka sasa Linamsaidia yeye pia watu wengine kupitia elimu anayoitoa ya Shamba Darasa kwa wakazi wa eneo analoishi huko Morogoro. na kusisitiza kuwa na matumizi Bora ya Ardhi.
  Mmoja 
wa Washiriki Akichangia Mada juu ya rushwa kuwa ni kikwazo kikubwa sana 
kwa wakulima na kuwa kuna Baadhi yao wanamazao mazuri lakini kutokana na
 kuwa mkulima mdogo anashindwa kuuza mazao yake na badala yake anayeuza 
mazao hayo ni Mkulima mkubwa ambaye huweza kutoa hongo na Mazao yake 
kununuliwa kirahisi 
Mshindi wa Shindano la Maisha Plus 2014 Boniface akitoa maelezo na kuchangia katika Mdahalo huo
 Tajiel Urioh kutoka Forum CC akihitimisha Mdahalo huo 
 Washiriki wakiendelea kufuatilia kwa makini Mdahalo huo 
  Kila mmoja akiwa makini kuhakikisha anapata Somo na kulielewa ili apate kwenda wafundisha na wengine.
 
  Washiriki wakiwa katika Mdahalo huo 
No comments:
Post a Comment