MBUNGE MGIMWA ;VYOMBO VYA HABARI ELIMISHENI JAMII JUU YA KATIBA MPYA
Mwenyekiti
wa kamati ya harambee ya kuichangia radio Maria mkoa wa Iringa
Paschal Bella kushoto akimpongeza mbunge wa jimbo la kalenga Godfrey
Mgimwa kwa kuichangia radio maria Tsh milioni 1.5 leo alipokuwa
mgeni rasmi katika harambee hiyo
Mbunge Mgimwa akipongezwa baada ya kuchangia milioni 1.5 radio Maria leo
Mbunge wa Kalenga Bw Mgimwa akikabidhi lapto kwa mlezi wa kwaya Msindo mzee Mtandi (P.T)
Mtandi akifurahi na mbunge wake Mgimwa
Furaha ya kukabidhiwa lapto
Mbunge wa
jimbo la kalenga Godfrey Mgimwa akivishwa kitenge cha Radio maria na
mwenyekiti wa kamati ya kuchangia radio Maria Iringa Paschal Bella
kushoto na katibu wake Martin Simangwa leo
Mgimwa akipongezwa
VYOMBO
vya habari zatakiwa kuepuka kupotosha umma juu ya mchakato
mzima wa bunge la katiba lililomalizika jana mjini Dodoma.
Kauli
hiyo imetolewa leo katika viwanja vya kanisa la Rc Mshindo na
mbunge wa jimbo la kalenga Godfrey Mgimwa wakati akichangia kiasi
cha Tsh milioni 1.5 wakati wa harambee ya kuichangia radio Maria .
Alisema
kuwa iwapo vyombo vya habari zitatumika vibaya kuna uwezekano
wa Taifa kuingia katika machafuko kama zilizo nje nyingine na kama
vyombo vya habari vitafanya kazi yake kwa kuzingatia misingi ya
maadili jamii itaunganishwa na vyombo hivyo.
“
Radio Maria ni moja kati ya radio ambazo nimekuwa nikizifuatilia
toka nikiwa mdogo na nimekuwa nikipenda zaidi jinsi radio hiyo
inavyofanya shughuli zake na mbali ya kufanya kazi ya kueneza
injili bado imekuwa msaada mkubwa katika kuelimisha umma……. Hivyo
rai yangu kwa radio maria ni kuona inaendelea hivyo hivyo na
ikiwezekana kuandaa vipindi kwa ajili ya elimu kwa umma juu ya katiba
mpya “
Alisema
kuwa wajumbe wa bunge la katiba wametimiza kazi yao ambayo umma
ulitegemea kutoka kwa wajumbe hao hivyo kazi iliyobaki ni ya
wananchi kucha kuipitisha katiba hiyo mwaka 2016 na kuwa kwa wakati
huu ni vema vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa umma juu
ya kazi nzuri iliyofanywa na bunge hilo la katiba .
Hata
hivyo alisema ni vema watanzania kuepukana na watu wachache
wasiolitakia mema Taifa ambao wanataka kuona nchi haitawaliki kwa
kutaka maandamano yasio na tija kwa jamii.
Mgimwa
alisema kuwa njia pekee ya kuepukana na viongozi wasio litakia
mema taifa ni pale ambapo vyombo vya habari vitakapoweka msimamo wa
uzalendo kwa kuepuka kuwa sehemu ya kuhamasisha kuvunjika kwa amani
nchini.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya harambee hiyo Bw Pascal Bella
akishukuru kwa mchango huo wa mbunge Mgimwa alisema kuwa mbali
ya kuwa mbunge huyo ni wa jimbo la kalenga ila amekuwa msaada
mkubwa kwa kufanikisha zoezi hilo la kuichangia radio hiyo.
Bella
alisema kuwa kila mwaka na kila wakati wadau wa Radio maria
wamekuwa na utaratibu wa kuichangia radio hiyo ambayo uendeshaji
wake unategemea michango kutoka kwa wadau mbali mbali na kuwa kwa
mwaka huu mkoa wa Iringa pekee unataraji kuchangia zaidi ya Tsh
milioni 30
No comments:
Post a Comment