RAILA ODINGA ATANDIKWA BAKORA
Mzee Mdzombo anasemekana kutokuwa timamu kiakili
Kiongozi
wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amemsamehe mzee aliyempiga bakora
katika mkutano wa hadhara wa kisiasa katika jimbo la Kwale Pwani ya
Kenya,
Mwanamume huyo, Lengo Mdzombo, anayefanya kibarua katika shamba moja Kwale, alikamatwa Jumanne na kufikishwa mahakamani.
Alishitakiwa kwa kosa la kumshambulia kiongozi huyo pamoja na gavana wa Kwale.BBC
Hali ya
taharuki ilitanda katika mkutano wa hadhara Jumatatu wiki hii baada ya
Mdzombo kwenda ukumbini na kuanza kumtandika bakora kiongozi wa upinzani
Raila Odinga pamoja na wanasiasa wengine.
Raila
alikuwa amejiunga na kikundi cha wanawake waliokuwa wanacheza densi ya
kitamaduni kuwatumbuiza wageni, pamoja na gavana wa jimbo la Kwale Pwani
ya Kenya Salim Mvuruya katika mkutanmo wa kisiasa.
Raila
alikuwa ameambatana na viongozi wengine, wakiwemo, Seneta Juma Boy,
Hassan Omar, Agnes Zani, James Orengo, Johnstone Muthama na wengineo.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga
Mzee huyo
alimpiga bakora Odinga ambaye ni waziri mkuu wa zamani kabla ya
kumgeukia gavana wa jimbo hilo na kumchapa mara mbili. Hata hivyo
mwanamume huyo alishindwa nguvu na walinzi wa Raila Odinga.
Polisi walithibitisha kuwa walimkamata mwanamume huyo na kumwachilia baada ya kugundua kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili.
Haijulikani
kwa nini mwanamume huyo alimshambulia Raila ila baadhi wanasema ni kwa
sababu alighadhabishwa pale waziri mkuu alipocheza densi na mwanamke
aliyesemekana kuwa mke wake ambaye alikuwa katika kikundi cha wanawake
waliokuwa wanawatumbuiza wageni waheshimiwa.
Viongozi waliofika walilazimika kusitisha densi hiyo kabla ya mwanamume huyo kushindwa nguvu
No comments:
Post a Comment