GREEN WASTE PRO LTD YAKABIDHI MAKASHA YA KUHIFADHIA TAKA.
Mwalimu
Mkuu wa shule ya msingi Bunge Bi. Khadija Telela, akizungumza na Meneja
wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena
aliyeambata na Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd,
Naima Mpili (kulia) waliofika shuleni hapo kukabidhi rasmi makasha ya
kuhifadhia taka.
Meneja wa
uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena, akielezea
nia ya kampuni yake kuendelea kusaidia shughuli mbalimbali za mazingira
katika shule hiyo kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Bunge Bi. Khadija
Telela (kushoto).(Martha Magessa)
Pamoja na
sababu za wanafunzi hao na mwalimu wao katika kutoa kipaumbele
mazingira, kuwa chanzo cha kutolewa kwa makasha hayo, sababu nyingine
iliyozingatiwa ni kuwa shule hiyo ipo katika kata ya Kivukoni ambapo
kampuni hiyo inazabuni ya kufanya usafi.
Amesema
wana mpango wa kuwapatia vifaa vya aina hiyo kwa shule nyingine
zinazofanya vyema kwenye usafi wa mazingira ila kwa sasa wameanza na
shule ya Bunge.
Mwalimu
wa mazingira wa shule hiyo, Frida Madanganya ameshukuru kampuni hiyo kwa
kuendelea kuwasaidia na anawategemea wataendelea zaidi kuhakikisha
kwamba shule hiyo inakuwa namba moja kwa utunzaji wa mazingira.
Naye
Mwalimu Mkuu Khadija Telela alisema shule yake ina changamoto kubwa hasa
maji ya Dawasco kwani maji yao ni yachumvi kwa kisima walichochimba.
Alisema maji hayo yana chumvi lakini juhudi zinaendelea kupata maji ya Dawasco.
Aidha aliwataka wanafunzi waliosoma hapo kuikumbuka shule hiyo kwani wengi wana uwezo wa kuifanya iendelee kuwika.
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI
ya Usafi ya Green Waste Pro imetimiza ahadi yake ya kuipatia shule ya
Msingi Bunge makasha ya kuhifadhia taka na vifaa vya usafi wa mazingira
iliyoitoa mwaka jana.
Mwaka
jana wakati wanafanya shughuli ya kupaka rangi shule hiyo,kampuni hiyo
ilifurahishwa na mazingira ya shule jinsi yanavyotunzwa kiasi cha
kufanya maamuzi ya kuwapelekea vifaa vya mazingira na hasa makasha ya
kuhifadhia taka.
Kwa
mujibu wa Afisa uendeshaji wa kampuni hiyo Abdallah Mbena,ambaye ndiye
aliyekabidhi makasha hayo,maamuzi ya kuwapatia makasha yametokana na
jinsi klabu ya mazingira ya shule hiyo na mwalimu wao anavyochakarika
katika kuhakikisha usafi wa mazingira katika shule hiyo.
Mbena
alisema kwamba wamefarijika sana na juhudi zinazofanywa na mwalimu na
wanafunzi wake katika kuhakikisha kwamba wanatunza mazingira.
Mwalimu
wa klabu ya mazingira wa shule ya msingi Bunge, Mwalimu Frida Madanganya
akiwatembeza kukagua mazingira ya maeneo mbalimbali ya shule hiyo
Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena
aliyeambatana na Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro
Ltd, Naima Mpili kabla ya kukabidhi makasha hayo.
Mwalimu
wa klabu ya mazingira wa shule ya msingi Bunge, Mwl. Frida Madanganya
akimtambulisha Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd,
Abdallah Mbena kwa wanachama wa klabu ya mazingira wa shule hiyo wakati
wa hafla ya kukabidhi makasha ya kuhifadhia taka.
Meneja wa
uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena
akizungumza na wanafunzi wa klabu ya mazingira shule ya msingi Bunge na
kuwahamasisha kuendelea kutunza mazingira yao na hata majumbani pia ili
wawe mabalozi wazuri wa mazingira.
Kaka Mkuu
wa shule ya msingi Bunge na mwenyekiti wa klabu ya mazingira shuleni
hapo Joseph Zakayo (kulia) akitoa shukrani kwa kampuni ya Green Waste
Pro Ltd kwa kutoa msaada huo wa makasha matatu ya kuhifadhia taka.
Kushoto ni Mwalimu wa klabu ya mazingira wa shule ya msingi Bunge, Mwl.
Frida Madanganya akifuatiwa na Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya Green
Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena aliyeambatana na Afisa Rasilimali watu wa
kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima Mpili.
Meneja wa
uendeshaji wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena
akikabidhi rasmi moja kati ya makasha matatu ya kuhifadhia taka
yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa Mwalimu wa klabu ya mazingira wa shule
ya msingi Bunge, Mwl. Frida Madanganya. Kulia ni Afisa Rasilimali watu
wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima Mpili.
Baadhi ya
michoro iliyopo kwenye majengo ya shule ya msingi Bunge yanayohamasisha
utunzaji wa mazingira kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Wanafunzi
wa klabu ya mazingira shule ya msingi Bunge wakiagana na Meneja wa
uendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena
aliyeambatana na Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro
Ltd, Naima Mpili.
No comments:
Post a Comment