Uchungu wa wazazi hawa kwa watoto wao umefikia kiwango hiki
Kuna
 ukweli kwenye msemo wa waswahili unaosema “uchungu wa mwana aujuaye 
mzazi”, na ndio maana stori nnayokuletea huenda ikawa ngeni na hujawahi 
kukutana nayo, lakini wazazi hawa wameonesha namna walivyo na uchungu 
kwa vitendo na sio maneno pekee.
Stori kutoka Kenya inahusu kitendo cha 
wazazi kuamua kujichukulia jukumu la ulinzi wa eneo la shule ili 
kukabiliana na vitendo vya uhalifu ambavyo vimekuwa vinajitokeza mara 
kwa mara katika maeneo hayo.
Kila jioni Esuruan Awet ni moja ya 
wazazi hao ambao hujiunga na kikundi cha askari Polisi wa akiba kwa 
lengo la kupiga doria eneo la shule ya msingi Nakatong’wa, Mashariki mwa
 Turkana huko Kenya.
Eneo la shule hiyo limekuwa likikabiliwa
 na matukio ya kuvamiwa mara kwa mara kitendo kilichowafanya wazazi hao 
kujiunga na kikosi hicho kukabiliana na uhalifu huo.

No comments:
Post a Comment