Wanne wafariki katika ajali ya ndege, watano majeruhi

Watu wanne wamefariki katika ajali ya ndege iliyotokea saa chache zilizopita baada ya ndege ndogo kugonga jengo la uwanja wa ndege na kuwaka moto.
Ndege hiyo iligonga jengo la uwanja wa 
Wichita, Kansas Marekani na kusababisha vifo vya watu wawili waliokuwemo
 ndani kufariki ikiwemo rubani wa ndege, na watu wengine waliofariki 
waliokuwa ndani ya jengo.
Majeruhi watano katika ajali hiyo walipelekwa hospitali, watatu waliruhusiwa kutoka huku wengine wawili wakiendelea kutibiwa.
Kikosi cha askari wa zimamoto 
walipambana na moto huo na kuuzima ndani ya muda mfupi, na baadhi ya 
barabara za ndege uwanjani hapo zilifungwa japo ajali hiyo haikuathiri 
ratiba za ndege kutua na kuruka.
Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba watu 13 
japo idadi ya watu waliokuwemo ndani ya ndege haijafahamika, uchunguzi 
unaendelea ili kubaini chanzo cha ajali hiyo pamoja na thamani ya vitu 
vilivyoathirika kutokana na ajali hiyo
No comments:
Post a Comment