Wanafunzi Hong K. kukutana na serikali

Viongozi 
wa wanafunzi huko Hong Kong wamekubali kukutana na upande wa serikali 
kujadili malalamiko yao siku tano baada ya maandamano makubwa ya 
kupigania demokrasia.
Hiyo 
inafuatia mwaliko kutoka kwa mkuu wa utawala wa Hong Kong CY Leung. 
Alitoa taarifa hiyo muda mfupi kabla ya kumalizika kwa muda wa mwisho 
uliowekwa na wanafunzi hao waliotishia kuvamia majengo ya serikali iwapo
 mkuu huyo hatajiuzulu.
Muda wa mwisho uliowekwa na wanafunzi hao umemalizika salama.
Bwana Leung amesema atabakia madarakani na kuwaonya waandamanaji kuwa watapata matatizo iwapo watavamia majengo ya serikali.
Kumekuwa 
na makabiliano makali katika eneo la majengo ya serikali ambapo 
waandamanaji wamekuwa wakiendelea kudai uchaguzi wa haki mwaka 2017.BBC
No comments:
Post a Comment