TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, October 24, 2014

Ni wasanii gani wa bongo walimshtua Davido kwa shangwe kwenye Fiesta Dsm?

Davido 33
Unaambiwa weekend iliyopita kwenye Fiesta ya Dar es salaam mwimbaji Davido wa Nigeria alitumia dakika zake zote kutazama screen zilizokua zimewekwa nyuma ya stage ya Fiesta baada ya kusikia shangwe zilizokua zinapigwa baada ya Wakali wengine kupewa time ya kumiliki stage.
Alilazimika kutazama TV hizo kwa umakini baada ya kuona shangwe walilopata WEUSI ambapo mashabiki walikua wanaimba nyimbo zao kwa muda mrefu ambapo Davido kabla ya kuuliza alitumia muda mrefu kuwatazama kwa makini baada ya kushangazwa na shangwe walilokua wanapata WEUSI hawa.
DD
Baada ya Wakali hawa kumaliza show Davido alianza kuuliza ni kina nani na wana umaarufu kiasi gani ambapo mmoja wa marafiki zake amesema stori hazikuishia uwanjani kwenye Fiesta bali mpaka Hotelini Davido alionyesha kushangazwa na shangwe la WEUSI na kuwaongelea tena.
Hii itafanya idadi ya Wasanii wa bongo wanaofahamika na Davido iongezeke manake alipokuja juzi Tanzania alihojiwa muda mfupi tu baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege na kusema msanii pekee wa Tanzania anaemfahamu ni Diamond Platnumz.
Mengine aliyoyasema ni kwamba kwenye album yake mpya inayotoka mwanzoni mwa 2015 wameshirikishwa wasanii wachache kutoka Afrika ambao ni pamoja na Diamond na Mafikizolo na kwamba kuna wasanii wawili wakubwa wa kimataifa aliowashirikisha ambao hatowataja kwa sasa.

No comments:

Post a Comment