JK KUPEWA ‘KATIBA MPYA’ LEO

Stori: Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete, leo atapokea ‘Katiba Mpya’ inayopendekezwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Samuel Sitta, katika tukio linalotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Rais Jakaya Kikwete,
Bunge 
hilo maalum, lilihitimisha kazi yake ngumu ya kujadili rasimu ya katiba 
mpya iliyowasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya 
Katiba, Jaji Joseph Warioba Oktoba 4 mwaka huu, baada ya Kamati ya 
Uandishi chini ya Andrew Chenge kuwa imewasilisha katiba inayopendekezwa
 iliyokubaliwa na wajumbe kutoka Bara na Visiwani.
Katiba 
hiyo inayopendekezwa, ilipatikana licha ya baadhi ya wajumbe kutoka 
vyama vya upinzani kujitoa kwa madai ya kuburuzwa na wenzao wa chama 
tawala, kitendo kilichoibua mjadala wa kitaifa huku makundi mbalimbali 
yakipingana, wengine wakiwaunga mkono na wengine wakiwapinga.GPL(P.T)
No comments:
Post a Comment