TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, October 15, 2014

HELLEN GEORGE AIBUKA MSHINDI WA SERENGETI SUPER NYOTA DIVA 2014


Mshindi wa shindano la Serengeti Fiesta Super Nyota Diva 2014 Hellen George jijini Dar es Salaam, akionyesha makeke yake muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo.

Hellen George akifuta machozi muda mfupi baada ya kuibuka mshindi.

...Akiwa amejiinamia chini baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Dar es Salaam 2014 katika shindano la Serengeti Super Nyota Diva ndani lililokuwa likifanyika mapema leo ndani ya Ukumbi wa Sun Cirro Sinza jijini Dar es Salaam.(P.T)
 
Mchujo wa kumpata mshindi wa Serengeti Fiesta Super Nyota Diva kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, umefanyika leo mchana ndani ya Ukumbi wa Suncirro Shekilango, ambapo tayari vijana mbalimbali wamejitokeza kuchuana na hatua ya kwanza tayari imemalizika kwa kupata washindi 5, ambao watachuana ili kuhakikisha anapatikana mshindi mmoja atakayeingia kwenye fainali za shindano hilo ambalo linatarajiwa kufanyika Ijumaa hii ndani ya Ukumbi wa Suncirro kwa kushirikisha wasanii wote waliopatikana kwenye jumla ya mikoa 14, ambayo imepitiwa na Tamasha la Serengeti Fiesta 2014.
Mmoja wa washiriki wa Serengeti Super Nyota Diva, akiwania nafasi ya kuwa Diva wa Jiji la Dar mapema leo ndani ya Ukumbi wa Suncirro.
Jaji wa mashindano hayo, Elias Barnabas akitafakari jambo wakati mchujo huo ukiendelea.
Mmoja wa washiriki akionyesha uwezo wake katika kuimba.
Majaji wa shindano hilo kutoka kulia ni mtayarishaji wa nyimbo, Tudi Thomas, DJ Fetty na Elias Barnabas wakiwajibika kuhakikisha wanampata mshindi bora wa shindano hilo.
Baadhi ya washiriki wakimshangilia mwenzao wakati akitafuta nafasi ya ushindi jukwaani hapo.
Mmoja wa washiriki hao akikamua kuwania nafasi hiyo.
Washiriki walioingia kwenye tano bora ya Shindano la Serengeti Super Nyota Diva 2014 jijini Dar es Salaam, wakiwa jukwaani.
Mshiriki akiwania nafasi ya kuwa Super Nyota Diva wa mkoa wa Dar es Salaam.
Majaji wa mchujo huo, Barnaba na DJ Fetty wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kutaja washiriki walioingia kwenye tano bora.
Mrembo akiwajibika jukwaani kuwania nafasi ya kuwa Diva wa Dar.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia shindano hilo.
Mshiriki akiwa stejini mbele huku baadhi ya washiriki wenzake wakimshuhudia wakati akiimba.

No comments:

Post a Comment