FC Barcelona yaweka rekodi ya kucheza mechi 7 bila kufungwa goli
FC
Barcelona jana usiku ilicheza mechi yake ya 7 katika ligi kuu ya
Hispania bila kupoteza mchezo wowote, wakishinda mechi 6 na kutoa sare
moja.
Lionel
Messi alifunga goli lake 402 tangu aanze kucheza soka la ushindani na
baadae akamtengenezea Neymar aliyehitimisha ushindi wa 2-0 dhidi ya Rayo
Vallecano.(P.T)
Kutokana
na ushindi huo kikosi cha Luis Enrique sasa kimefanikiwa kuwa timu ya
kwanza katika historia ya La liga kucheza mechi 7 za mwanzoni mwa ligi
hiyo bila kuruhusu wavu wao kugushwa.
Pia wakati huo huo golikipa wa timu hiyo, Mchile Claudio Bravo ameweka rekodi mpya ya katika kulinda lango lake.
Bravo
amevunja rekodi ya kucheza dakika nyingi bila kuruhusu wavu wake
kuguswa, mpaka kufikia sasa Bravo amecheza jumla ya dakika 561 bila
kufungwa goli, akivunja rekodi ya golikipa wa zamani wa Barca, Pedro
Artola aliyecheza kwa dakika 560 bila kufungwa goli katika msimu wa
1977-78.
No comments:
Post a Comment