Msichana asimulia ya Boko Haram
Baadhi ya wasichana waliotekwa nyara
Ni miezi
sita sasa baada ya wanamgambo wa kiislam wa kundi la Boko Haram kuwateka
wanafunzi wasichana Zaidi ya 200 kaskazini mashariki mwa Nigeria,
wasichana watatu ambao wametoroka wamezungumza katika mahojiano maalum
na idhaa ya Kihausa ya BBC.
Tukio
hili linakuja wakati serikali ya Nigeria ikiwa katika makubaliano ya
kusimamisha mapigano dhidi ya Boko Haram hatua itakayo saidia
kuwaachilia huru wasichana waliotekwa na kundi hilo .
''
nilikuwa nataka kurukia nje wakati msichana mwenzangu aliponikamata kwa
nyuma na kusema watakupiga risasi kama utafanya hivyo. Nikasema, nini
utofauti wataniua mimi hapa na kuacha maiti yangu ikusachukuliwa
nilikuwa nalia na kuomba mpaka tulipoifikia kambini" Anasimulia msichana
mmoja alitoroka mikononi mwa Boko Haram.(P.T)
Akizungumza
katika mahojiano maalum na idhaa ya Kihausa ya BBC, Msichana huyu
anakumbuka jinsi alivyokuwa nyuma ya Lori wakati wanapinaji wa Boko
Haramu walipomteka yeye na wasichana wengine.
Zaidi ya
wasichana 200 kati miongoni mwao walikuwa walitekwa lakini wale
waliokimbia walibahatika kutoingia katika hofu kubwa kwenye mikono ya
watekaji.
Shirika
la kimataifa la kutetea haki za binaadam la Human Rights Watch limesema
wanawake wanaoshikiliwa na kundi la Boko Haramu wamekuwa wakinyanyaswa,
kubakwa na hata kulazimishwa kuolewa.
Katika
ripoti mpya ya shirika hilo inasema Wanamgambo hao wa Kiislam
wamewawateka wanawake Zaidi ya 500 na wasichana tangu mwaka 2009.
Serikali
ya Nigeria hivi karibuni imetangaza makubaliano ya kusimamisha mapigano
dhidi ya Boko Haram ambayo hatua itakayawafanya wanamgambo ho kuachilia
huru wasichana wa hao waliotekwa huko Chibok.
Lakini
Boko Haram wenyewe hawajawahi kuthibitisha makubaliano yoyote ya
kusitisha mapigano na hakuna dalili zozote za kuachiwa kwa wasichana
haohivi karibuni.
Lakini kwa wale waliobahatika kutoroka, matatizo ya kisaikolojia bado yanawasumbua..
No comments:
Post a Comment