Picha kumi za Ikulu zinazoongoza kwa matumizi mabaya ya fedha duniani
Kuna malalamiko mengi tumekuwa tukiyasikia kuhusu Ikulu za nchi kuhusishwa na ufujaji mkubwa ama matumizi mabaya ya fedha.
Hizi ni picha na orodha ya Ikulu tano zinazoongoza kwa matumizi makubwa zaidi ya fedha duniani.
No. 1-
Jumba jipya la Ikulu ya Uturuki, liko katika jiji la Ankara na kwa sasa
huenda likawa jumba kubwa zaidi kuliko Ikulu ya Marekani. Ujenzi wake
umegharimu zaidi ya Dola Mil. 350.
Muonekano wa jumba jipya la Ikulu ya Uturuki wakati wa Usiku.
No.2-
White House, Ikulu ya Marekani. Ikulu hii iko Washington D.C, na
imekuwa ikitumika kama Ikulu tangu mwaka 1800, Marekani ikiongozwa na
rais John Adams.
Muonekano wa White House wakati wa usiku.
No. 3-
Planalto, Ikulu ya rais wa Brazil. Iko katika jiji la Brasilia. Imekuwa
ikitumika kama Ikulu tangu mwaka 1960, wakati huo rais akiwa Oscar
Niemeyer.
Muonekano wa Planalto, Ikulu ya Brazil wakati wa usiku.
No. 4- Grand Kremlin, Ikulu ya Urusi iliyopo jijini Moscow. Imeanza kutumika kama Ikulu tangu mwaka 1849.
Muonekano wa Grand Kremlin, Ikulu ya Urusi wakati wa usiku.
No. 5- Jumba la Ikulu ya Taipei, Taiwan. Imekuwa ikitumika kama Ikulu tangu mwaka 1950.
Muonekano wa Jumba la Ikulu ya Taipei, Taiwan wakati wa usiku.
No comments:
Post a Comment