Mgonjwa wa Ebola agundulika Newyork
Mji wa Newyork
Daktari
wa Marekani aliyekuwa akiwahudumia wagonjwa wa Ebola Nchini Guinea
amepimwa na kukutwa na virusi vya ugonjwa huko katika hospitali ya ya
mjini Newyork.
Dr Craig
Spencer ambaye ni mmoja kati ya madaktari wasio na mipaka alianza
kujisikia maumivu na homa siku chache tu baada ya kurejea Marekani
akitokea Afrika Magharibi.BBC
Siku ya Alhamisi wiki hii Craig alipelekwa hospitali kwaajili ya vipimo na kisha akatengwa kwa uchunguzi zaidi wa afya yake.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari Meya wa mji wa Newyork Bill de Blasio
amesema watu hawapaswi kuwa na hofu kwani hatua zote mhimu zilifuatwa
katika kumchunguza Dr.Craig na hadi alipobainika kuwa na maambukizi
hayo.
Kubainika
kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola kwa Dr.Craig kunaongeza idadi ya
waliobainika kuwa na ugonjwa huo nchini Marekani kutoka watatu na
kufikia wagonjwa wanne.
No comments:
Post a Comment