Hukumu ya kifo yatangazwa kwa wanawake wanaojiuza pamoja na wateja wao
Katibu
wa maendeleo ya jamii katika jiji la Abuja Nigeria, ametangaza ‘kiama’
kwa wanawake wanaofanya ‘biashara ya kujiuza’ pamoja na wateja wao.
Taarifa iliyochapishwa na Today Internet Newspaper
imesema, katibu mkuu huyo Blessing Unoh amesema serikali imetoa amri ya
kusitisha biashara hiyo ndani ya saa 48, kwa yeyote atakayekiuka hatua
kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Amri hiyo imetolewa saa chache baada ya
katibu mkuu huyo kutembelea maeneo mbali mbali ambayo yamebobea kwa
biashara hiyo ambapo amejionea hali halisi iliyopo.
Aidha amesema kwa yeyote atakekiuka amri hiyo na kukutwa na hatia ya kutenda kosa hilo awe tayari kukabiliana na hukumu ya kifo.
No comments:
Post a Comment