Hawa ndio wanafunzi wanaofanya mitihani ya Sekondari wakiwa na mimba.
Afisa
 elimu katika kaunti ya Bungoma Kenya, ametoa taarifa kuhusiana na 
wanafunzi 53 wanaofanya mitihani wa kumaliza elimu ya sekondari 
iliyoanza siku ya Jumanne wiki hii, ni wajawazito.
taarifa iliyochapishwa na news 24 Kenya
 imesema Charles Anyika; mkurugenzi wa elimu wa kaunti hiyo amesema 
idadi hiyo imebainika baada ya kufanya uchunguzi, na kuongeza kuwa 
anategemea idadi ya wanafunzi wenye ujauzito ni kubwa kuliko 
iliyopatikana kwa kuwa baadhi ya wakuu wa shule walitoa taarifa za uongo
 na pia baadhi ya familia wamekuwa ‘wakimalizana’ na watuhumiwa bila ya 
kutoa taarifa.
Amesema awali kabla ya uchunguzi huo 
walitegemea idadi ya wanafunzi wenye mimba kufikia 100, wakati huo huo 
amewataka walimu wawaache wanafunzi hao wafanye mitihani yao kwa utulivu
 na kuwaagiza walimu kuandaa magari ambayo yatasaidia iwapo mwanafunzi 
yoyote atapata dharura.
Anyika amewataja walimu, waendesha 
‘bodaboda’, na wanaume waliooa ni wahusika wa mimba hizo na kuongeza 
kuwa umaskini ni chanzo kikubwa cha tatizo hilo, na kuwataka wazazi 
kuwalinda watoto wao na kuwapa elimu juu ya hatari ya mimba za utotoni 
pamoja na ngono zembe.

No comments:
Post a Comment