Huyu ndiye Rais wa kwanza mzungu ndani ya Afrika tangu kuisha ubaguzi wa rangi

Guy Scott ambaye alikuwa makamu wa rais 
Zambia wakati wa utawala wa Michael Sata ametajwa kushika nafasi ya 
urais wa nchi hiyo kwa sasa mpaka pale ambapo ataapishwa mara baada ya 
kufanyika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Waziri wa ulinzi Zambia Edgar Lungu 
amesema maandalizi ya uchaguzi huo yataanza muda wowote ambapo katiba ya
 nchi hiyo inaagiza kufanyika uchaguzi wa Rais ndani ya siku 90 baada ya
 kufariki kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo.
Scott ameteuliwa kushika wadhifa huo 
ambapo hii itakuwa mara ya kwanza kwa rais mzungu kuongoza nchi ya 
Afrika tangu kuisha kwa kipindi cha ubaguzi wa rangi Afrika Kusini chini
 ya utawala wa FW de Klerk.
Kulikuwa na utata uliotokana na katiba 
ya Zambia kumruhusu Scott kushika wadhifa huo kwa sababu wazazi wake 
wanatokea Scottland, huku katiba hiyo ikitaja rais wa nchi hiyo ni 
lazima awe Mzambia kamili kwa maana ya kwamba wazazi wake wote wawili 
wanapaswa kuwa wamezaliwa nchini humo
No comments:
Post a Comment