SHIRIKISHO LA MUZIKI TANZANIA LATOA PONGEZI KWA BUNGE MAALUM LA KATIBA
Na Anitha Jonas –Maelezo.
SHIRIKISHO
la Muziki Tanzania limetoa pongezi za dhati kwa Bunge Maalum la Katiba
lililokuwa likiongozwa na Mwenyekiti wa Bunge hilo Mhe. Samuel Sitta kwa
kuingiza Ibara tatu katika Rasimu ya Katiba inayopendekezwa huko mjini
Dodoma.
Pongezi
hizo zilitolewa jana na Rais wa Shirikisho hilo Bw. Addo November
alipokuwa akiongea na Waandishi wa habari hapo jana huku akisema kuwa
Rasimu Inayopendekezwa imezingatia haki za Wasanii kwa kuingiza Ibara
tatu zikiwemo Ibara ya 15, ya 38 (II) na Ibara ya 56, 3 (e) ambazo Ibara
hizo zinalinda kazi za muziki na sanaa zote kwa ujumla.(Martha Magessa)
Bw.
November alieleza kuwa Shirikisho limefurahi kuona kuwa Sheria ya
inayohusu masuala ya kazi za sanaa katika nchini imeanza kutekelezwa
Kikatiba kama ilivyo katika nchi mbalimbali zikiwemo Marekani, Rwanda na
Uingereza.
"Kwa
kubainisha ibara hizi katika Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa,
zinaonyesha ulindaji wa Hati Miliki (Intellectual property) za Wasanii
na kazi zao na hii itasaidia kuboresha maisha ya wasanii kimapato kwa
kupitia kazi zao kwani Katiba hii itawalinda wasanii Kisheria", alisema
November.
Aliongeza
kuwa Shirikisho limeingia Mkataba na Kampuni ya JB Belmont kwa kuweza
kuwapatia wasanii na waandishi wa habari punguzo la bei katika huduma
mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.
Aidha,
November aliwashauri waandishi wa habari kuunda Shirikisho la Waandishi
wa habari la muziki kwani hii itasaidia kupata na kutoa taarifa
mbalimbali kwa jamii zinazohusu masuala ya muziki kwa kuaangalia
walikotoka na wanakoelekea kimaendeleo.
Naye
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya JB Belmont, Bi. Gillian Macheche alisema
kuwa kutakuwa na punguzo la asilimia 40 kwa huduma mbalimbali ikiwemo
kukodi Ukumbi wa Mkutano, Vyumba vya kulala wageni, vyakula na Vinywaji
kwa wasanii na waandishi wa habari.
Kwa
upande mwingine Mjumbe wa Shirikisho hilo ambaye pia ni Mwanamuziki
mkongwe nchini Bw. Kassim Mapili alitoa shukrani zake za dhati kwa
waandishi wa habari kwa kutoa taarifa kwa umma juu ya afya yake pamoja
na jamii kwa ujumla kwa kumsaidia katika kipindi chote alichokuwa
akitibiwa ugonjwa wa Moyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
No comments:
Post a Comment