TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, October 7, 2014

Viboko vyatembezwa makaburini Sengerema

M
Wajukuu wa marehemu Sabina Ngalu wa Mwanza wamecharazwa viboko na watoto wa marehemu baada ya kung’ang’ania kaburini wakitaka wapewe fedha.
Chanzo cha wajukuu hao zaidi ya 10 kucharazwa bakora ni kung’ang’ania ndani ya kaburi lililokua limeandaliwa kwa ajili ya kuhifadhi mwili wa marehemu wakitaka wapewe ng’ombe mmoja au sh.100,000 kama zinavyotaka mila za kabila la kisukuma.
Gazeti la MTANZANIA ambalo lilikua shuhuda katika eneo hilo lilisema kitendo hicho kilimkera Padri Nicodemus Mayalla aliyekua eneo hilo huku akiwataarifu polisi kuhusu vurugu hizo hata hivyo kaka mkubwa wa marehemu aliamua kuchukua fimbo na kuanza kuwachapa.
Kitendo cha kuwachapa kiliamsha hasira zaidi kwa wajukuu hao ambao nao walijibu kwa kurusha michanga wakiwa ndani ya kaburi hadi waombolezaji walipoamua kuchanga na kuwapa fedha hizo ndipo walipotoka.
Hata hivyo Padri huyo aligoma kurejea eneo la makaburi kuongoza ibada hadi hapo watoto hao watakaporudisha fedha hizo na kuomba radhi,jambo ambalo lilitekelezeka.

 

No comments:

Post a Comment