Hii ndiyo taarifa iliyotolewa na FIFA kuhusiana na Ebola
Shirikisho
la soka Duniani FIFA limesema mashindano ya kombe la dunia la FIFA kwa
ngazi ya vilabu yanayotarajiwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu
yataendelea kama ilivyopanga, huku likisisitiza vilabu vyote kuhusiana
na kuchukua tahadhari juu ya virusi vya Ebola pindi inapofanyika
michuano hiyo ya kimataifa.
Kitendo cha baadhi ya nchi kukumbwa na
janga la Ebola kuliibua maswali namna ambavyo michuano hiyo itawezekana
kufanyika na pia juu ya usalama wa wachezaji hasa pale ambapo
watalazimika kwenda kucheza mechi katika moja ya nchi ambayo iko kwenye
ukanda ulioathirika na ugonjwa huo.
FIFA imewatoa wasi wasi kwa kutoa ushauri namna ambayo itasaidia kupunguza hatari ya kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa huo.
Mbali ya mapendekezo yaliyotolewa na
FIFA ya kufanya vipimo vya afya za wachezaji wa vilabu husika baada ya
kurejea kutoka moja ya nchi ambayo iko katika ukanda ulioathiriwa na
Ebola, na kushauri naadhi ya mechi ambao zilipangwa kufanyika Guinea,
Sierra Leone na Liberia kuhamishiwa katika viwanja ambavyo vipo katika
nchi zenye viwanja vyenye nafasi.
Mbali na FIFA kusisitiza kuwatenga
haraka wachezaji watakaoonesha dalili za Ebola wakati ikifanyika
michuano ya kimataifa, vile vile imewataka wachezaji kutoka nchi
zilizoathirika kuwa na tahadhali kubwa kwa kupima afya zao.
No comments:
Post a Comment