T.I amehojiwa tena Marekani na kuzungumzia mengine mapya kuhusu Tanzania
Clifford
Joseph Harris, Jr. a.k.a T.I mkali kutoka Marekani aliyeangusha show ya
nguvu katika jukwaa la Fiesta 2014 siku ya Jumamosi Oktoba 18 2014
katika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam, bado ameendelea
kuyasimulia mazuri na makubwa ya kuvutia aliyokutana nayo Tanzania.
Katika mahojiano aliyofanya New York Marekani na kituo maarufu cha redio Power 105.1
kwenye show ya Breakfast Club, T.I amesema tangu aanze kufanya muziki
hajawahi kufanya show kwenye jukwaa lolote mbele ya mashabiki zaidi ya
50,000.
T.I amelinganisha idadi hiyo kubwa
aliyokutana nayo Tanzania kuwa ni sawa na kufanya show katika uwanja wa
mpira wa miguu na kuujaza kwa show moja, kitu ambacho anakiona kabisa
sio rahisi na ndio maana hii ya Leaders imekua kubwa kwake.
Swali la kuhusu Ebola bado liliulizwa
kwa T.I kama alichukua tahadhari kwa kufanya utafiti kabla ya kwenda
Afrika na kusema hakuwa na hofu yoyote alipokuja Tanzania, zaidi alikuwa
akifikiria tu kuhusu mpenzi wake, hata hivyo hakukutana na Ebola wala
kuona hata dalili za uwepo wake na kusisitiza kwamba mara nyingi Ebola
imekua ikiwapata Wanaowahudumia wagonjwa’
Kwenye sentensi nyingine rapper huyu
mwenye umri wa miaka 34 alisifia jinsi alivyopokelewa vizuri na kusema
Tanzania ni watu wazuri hivyo akamwambia Dj Envy kwamba ataenjoy sana
kwenye safari yake ya Afrika December mwaka huu.
No comments:
Post a Comment