UEFA kuamua mechi ya Man City na CSKA
Mchezaji wa Mancity Yaya Toure
Kilabu ya soka nchini Uingereza
Manchester City imesema kuwa itabaini siku ya ijumaa iwapo mechi kati
yake na kilabu ya Urusi CSKA Moscow itachezwa katika uwanja usio na
mashabiki.
CSKA kwa sasa wanahudumia marufuku ya uwanja wao baada ya visa vitatu vya ubaguzi wa rangi na ghasia kuripotiwa.
Mabingwa
hao wa Urusi walicheza mechi yao ya kwanza katika uwanja wa nyumbani
katika kundi E dhidi ya Bayern Munich katika uwanja uliokuwa hauna
mashabiki.
Shirikisho
la soka barani Ulaya UEFA litakutana kuamua iwapo mechi ya Manchester
City mjini Moscow ifikiapo tarehe 21 mwezo Octoba itawaruhusu mashabiki
au la.BBC
Mashabiki wa CSKA Moscow nchini Urusi.
Tukio la
ghasia za hivi karibuni zilizoshirikisha Mashabiki wa CSKA lilikuwa
katika ufunguzi wa mechi ya klabu bingwa barani Ulaya mjini Roma mnamo
tarehe 17 mwezi Septemba.
Mashabiki
wa Urusi walishiriki katika ghasia hizo na polisi ambapo walirusha
cheche za moto katika uwanja wa Stadio Olimpiko baada ya kushindwa kwa
mabao 5-1.
Ghasia
hizo zinajiri baada ya matukio mawili tofauti ya ubaguzi wa rangi katika
mechi za klabu bingwa barani ulaya ikiwemo mechi moja kati ya CSKA na
City ambapo Yaya Toure alilalamika kuhusu ubaguzi wa rangi mnamo mwezi
Octoba.
Timu hiyo
ya Urusi ilipoteza kwa bao moja kwa bila dhidi ya Bayern siku ya
jumanne katika mechi ya iliochezwa katika uwanja mtupu
No comments:
Post a Comment