Boko Haram yateka wanawake wengine
Taarifa iliyoripotiwa na shirika la utangazaji Uingereza BBC
 imesema kikundi cha wapiganaji cha Boko Haram kimefanya mashambulizi 
katika kijiji cha Adamawa kilichopo Kaskazini Magharibi ya Nigeria na 
kuteka wanawake na wasichana katika kijiji hicho.
Utekaji wa wasichana na wanawake hao 
unatokea ndani ya siku sita tangu serikali ya Nigeria na kikundi hicho 
walipofanya makubaliano ambapo Boko Haram waliahidi kuwaachilia huru 
zaidi ya wasichana 200 wanaoshikiliwa na kikundi hicho.
Japo Boko Haram wamekiuka makubaliano 
waliyoafikiana Ijumaa iliyopita, bado serikali ya Nigeria ina matumaini 
ya kuachiliwa huru kwa wasichana hao baada ya kikao kinachotarajiwa 
kufanyika muda wowote kuanzia sasa huko Chad

No comments:
Post a Comment