DK. SHEIN AMFUTA KAZI MWANASHERIA MKUU SMZ

RAIS wa 
Zanzibar na Mweneykiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein 
amemteua Mh. Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.
Kwa 
mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi 
ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee, Dkt Shein 
amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 55(1) 
cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Mheshimiwa
 Said Hassan anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar 
Mh. Othman Masoud Othman ambaye Uteuzi wake umefutwa kwa mujibu wa 
Vifungu vya 53, 54 (1) na 55 (3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 na 
Kifungu 12(3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.
Kabla ya Uteuzi huo Mheshimiwa Said Hassan Said alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Uteuzi huo umeanza tarehe 07, October, 2014IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 
(Martha Magessa)
No comments:
Post a Comment