Kilichomkuta ‘aliyemdiss’ refa wa kike
Makamu
wa Rais wa shirikisho la mpira wa miguu kaunti ya Northumberland,
Uingereza John Cummings amesimamishwa kwa kipindi cha miezi 4 kwa kosa
la kumwambia mwamuzi wa kike kuwa sehemu anayopaswa kuwapo mwanamke ni
jikoni na sio katika uwanja wa mpira wa miguu.
Cummings amemtolea kauli hiyo mwamuzi
Lucy May, kwamba hawezi kuhimili kazi ya kuwa mwamuzi, na kuongeza kuwa
katika maisha yake yote hakuwahi kuona mwanamke akichezesha mpira wa
miguu.
Tume huru ya uratibu wa shirikisho la
mpira wa miguu imesema kuwa Cumming amekiuka kanuni za mpira wa miguu za
shirikisho hilo kwa kutumia lugha ya kukashifu na ubaguzi wa kijinsia.
Makamu huyo wa rais amekiri kuwa hakuwa
anamaanisha kwenye kile alichokizungumza bali ilikuwa ni utani ambao
huenda May hajauchukulia hivyo, japo chama hicho kimesema nafasi ipo
wazi kwa refarii huyo kukata rufaa juu ya hukumu hiyo.
Hukumu aliyopewa refa huyo inaambata na adhabu ya faini ya paundi 250 na pia adhabu ya kuhudhuria mafunzo.
Mkurugenzi wa chama cha soka
Northumberland, Clive Oliver amekemea kitendo hicho na kusema mpira wa
miguu unajumuisha watu wote na hakuna ubaguzi wowote unaopaswa
kuvumiliwa
No comments:
Post a Comment