ZEIDAN AKANUSHA KUFUTWA KAZI

Aliyekuwa waziri mkuu wa Libya, Ali 
Zeidan, amepuuzilia mbali kura ya kutokuwa na imani naye iliyotangazwa 
na Bunge la taifa hilo mapema juma hili iliyopeleekea kufutwa kwake.
Ameiambia shirika la habari la Channel
 France 24 kuwa kura hiyo ya kutokuwa na imani naye illikuwa imejengwa 
kwa misingi ya uwongo huku pia akikanusha madai ya ufisadi dhidi ya 
serikali yake.
Ali Zeidan aliondolewa Ofisini mnamo 
siku ya Jumanne baada ya meli ya mafuta kutoka bandari inayodhibitiwa na
 waasi kufaulu kuvunja nanga ya wanajeshi wa wanamaji wa Libya kuingia 
bahari kuu na kutoroka.
Bwana Zeidan alifaullu kuondoka nchi hiyo licha ya kupingwa marufuku ya kutosafiri nje ya taifa.(P.T)
No comments:
Post a Comment