Mchezo wa Yanga vs Al Ahly wahamishwa, sasa kupigwa mji huu
Baada
ya utata juu ya ni sehemu gani utakaofanyika mchezo wa marudiano kati
ya wenyeji Al Ahly dhidi ya wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye
mashindano ya Kimataifa Young Africans huku ikiwa iebakia siku tatu
kabla ya mchezo, maamuzi ya shirikisho la soka nchini Misri yameamulu
mchezo huo utafanyika mjini Alexandria katika Uwanja wa Border Guard
stadium (Haras el Hadod)
Taarifa ya Chama cha Soka nchini Misri imesema mchezo huo ambao awali
ulikua ufanyike katika jiji la Cairo sasa utafanyika katika mji wa
Alexandria takribani kilometa zaidi ya 200 kutoka Cairo ambapo kikosi
cha Young Africans kimeweka kambi kujiandaa na mchezo huo.
Mara baada ya kupata taarifa hizo kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini
Misri, uongozi wa Young Africans uliopo jijini Cairo ukiongozwa na
makamu mwenyekiti Clement Sanga ambaye pia ndio mkuu wa msafara, tayari
umeanza maandalizi ya kuhakikisha timu inakwenda mjini Alexandria
kucheza mchezo huo wa jumapili na kufanya vizuri.
Ni jambo la kushangaza taarifa za Uwanja zinatolewa siku tatu kabla
ya mchezo huku fika wahusika wakitambua kuwa Young Africans ilifahamu
mchezo huo utafanyika Cairo takribani wiki mbili zilizopita viongozi wa
Al Ahly waliopokuwa nchini Tanzania walidhibitisha hilo.
Pamoja na mabadiliko hayo ya ghafla ya sehemu utakapofanyika mchezo
siku ya jumapili, benchi la ufundi pamoja na wachezaji na viongozi
waliopo jijini Cairo bado wana imani ya kufanya vizuri na kusonga mbele
katika hatua ya 16 bora.
Wakati huo huo washambuliaji wawili wa timu ya Taifa ya Uganda Hamisi
Kizza na Emmanuel Okwi tayari wameshawasili jijini Cairo majira ya saa 7
usiku kwa shirika la ndege la Egypt Air wakitokea nchini Zambia
walipokuwa wakiiwakilisha timu yao ya Taifa kwenye mchezo wa kirafiki
jana siku ya jumatano.
Wachezaji hao mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndege moja kwa moja
wameungana kambini na wachezaji wengine katika Hoteli ya Nile Paradise
Inn kuendelea na maandalizi ya mchezo huo wa jumamosi.
Mchezo huo wa siku ya jumapili ambao unafanyika mjini Alexandria
katika Uwanja wa Border Guard Stadium (Haras El Hadod) hautakua na
watazamaji kutokana na mamalaka ya ulinzi na usalama kuzuia mashabiki
kuingia katika mchezo wowote wa mpira wa miguu nchini Misri.
SOURCE: YANGA WEBSITE - http://youngafricans.co.tz
No comments:
Post a Comment