100 wakamatwa mjini Mombasa, Kenya

Watu 100 wamekamatwa mjini Mombasa 
Pwani ya Kenya kufuatia mashambulizi yaliyofanywa ndani ya kanisa moja 
mjini humo siku ya Jumapili. Watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki na 
kufunika nyuso zao waliwapiga risasi waumini wa kanisa moja mtaani 
Likoni na kuwaua watu wanne Watu  walifariki papo hapo wengine 
wakifariki hospitalini wakati wakipokea matibabu. Wengine 17 
walijeruhiwa vibaya.
Polisi wanasema kuwa watu watatu 
waliokuwa wamejihami walivamia kanisa la Joy Jesus na kuanza 
kuwafyatulia waumini risasi kiholelea. Kadhalika polisi walisema kuwa 
washukiwa wakuu wa shambulizi hilo wametoweka (J.G)
Hakuna mtu yeyote aliyekiri kufanya 
mashambulizi hayo , ila Kenya imekuwa ikishuhudia ongezeko la 
mashambulizi tangu kuanza kujihusisha na vita nchini Somalia mwaka 2011.
 Jeshi la Kenya linasaidiana na wanajeshi wa Muungano wa Afrika 
kupambana na kundi la wanamgambo la Al Shabaab.
Hali ya usalama imedhibitiwa mjini 
humo kufuatia shambulizi hilo ambalo limekuja siku chache tu baada ya 
polisi kunasa washukiwa watatu wa ugaidi wakiwa na mabomu mawili makubwa
 tayari kufanya shambulizi kubwa. Pia walinasa vilipuzi vingine ndani ya
 gari lililokuwa limeegeshwa karibu na kituo cha polisi. Mji wa Mombasa 
wenye sifa ya utalii, umekuwa ukikumbwa na suitofahamu ya kiusalama 
kutokana na vijana wengi kujiunga na itikadi kali za dini hiyo.
No comments:
Post a Comment