KAMPUNI KUBWA YA NDIZI YAZINDULIWA
Kampuni kubwa ya matunda nchini
Ireland, Fyffes na kampuni nyingine hasimu ya Marekani Chiquita
zimeungana kubuni kampuni kubwa zaidi ya kuzalisha Ndizi duniani yenye
thamani ya dola bilioni moja.
Kampuni hiyo mpya itajulikana kama
ChiquitaFyffes na inatarajiwa kuuza kati ya maboxi milioni 160 ya Ndizi
kila mwaka kuliko kampuni nyingine yoyote duniani.
"hii ni hatua kubwa kwa kampuni za Chiquita na Fyffes ambazo zinaleta pamoja kampuni nzuri zaidi za kuzalisha Ndizi duniani,'' alisema mkuu wa kampuni ya Chiquita, Ed Lonergan.
Ushirikiano huo utashuhudia wenye hisa wa kampuni hiyo wakipata hisa huku wamiliki wa Fyffes wakimiliki asilimia 49.3% ya kampuni hiyo.
Bwana Lonergan alisema kuwa ushirikiano huo utasaidia kuokoa matumizi ya pesa na kueneza maeneo ya kuuza matunda hayo.
Ushirikiano huo ulifanyika huku kampuni ya Fyffes ikitangaza faida zake kabla ya kutozwa kodi mwaka 2013 ilipanda kwa asilimia 9.8% hadi pauni milioni 23.8.
Ilisema kuwa licha ya faida kushuka ikilinganishwa na mwaka 2012, biashara sio mbaya sana.
Iliongeza kuwa mfumuko wa bei ya matunda hayo na uthabiti wa dola ya Marekani dhidi ya Pauni iliathiri biashara ya matunda hayo.(E.L)

No comments:
Post a Comment