TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, March 10, 2014

Kamati Kuu CCM yakutana Dodoma 

ccm_de638.jpg
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipowasili mkoani Dodoma jana. Wengine ni Makamu wa Rais, Dk Mohamed Bilal na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Dodoma. Rais Jakaya Kikwete, jana aliwasili mjini Dodoma katika kipindi ambacho Bunge Maalumu la Katiba liko njiapanda baada ya wajumbe kushindwa kuafikiana kama upigaji wa kura uwe wa siri au wa wazi.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenye wajumbe wengi katika Bunge hilo kimeweka msimamo wa kitaasisi kutaka kura ya wazi ilihali vyama vya upinzani na baadhi ya wajumbe kutoka kundi la wajumbe 201 walioteuliwa na Rais wakitaka kura ya siri.

Pia baadhi ya wajumbe wanaotokana na CCM wakiwamo wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar nao wameshikilia msimamo wa kutaka kura ya siri.
Ingawa taarifa kutoka CCM zilidokeza kuwa ujio wa Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM ni mahususi kwa ajili ya kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), suala la kura linaweza kugusiwa.
Taarifa hizo zinadai agenda kuu ya CCM hiyo ni kupitisha jina la mgombea ubunge katika Jimbo la Chalinze mkoani Pwani ambapo mjumbe wa NEC ambaye ni mtoto wake, Ridhiwan Kikwete aliongoza kura za maoni kwa kuwashinda Imani Madega na Ramadhani Maneno.
Habari kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Mashauriano, zilieleza kuwa kamati hiyo imeshindwa kufikia mwafaka kuhusu utaratibu gani utumike katika upigaji wa kura na mtu anayetegemewa kukoa jahazi ni Rais Kikwete.
"Jana (juzi) walituambia kuwa kwa vile Rais angewasili leo (jana) basi wanaomba muda wafanye mashauriano naye na ikibidi waangalie uwezekano wa kuitisha mkutano wa ndani wa chama wa dharura kujadili hili jambo," alidokeza mjumbe mmoja.
Mjumbe huyo aliyeomba jina lake lihifadhiwe, alisema baada ya kukutana na Rais, wajumbe wa kamati hiyo ya mashauriano wanaotokana na CCM watawasilisha mrejesho wa nini wamekubaliana kwenye kikao ili leo, vifungu 37 na 38 ambavyo vimekwama viweze kuridhiwa.
Chanzo, mwananchi (R.M)

No comments:

Post a Comment