TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, March 22, 2014

Mazungumzo ya amani Sudan Kusini yacheleweshwa 

 Wawakilishi wa waasi wa Sudan Kusini wakizungumza na mwakilishi wa Marekani kwa Sudan Kusini, Donald E. Booth

Serikali ya Sudan Kusini imeweka wazi kuwa haitaki kushiriki katika utaratibu wa amani kama kundi la viongozi wa zamani wa kisiasa wenye vyeo vya juu ambao serikali iliwakamata baada ya mapigano kuzuka mwezi Disemba watajiunga na mazungumzo kama kundi la tatu.
Waziri wa zamani na mfungwa wa kisiasa, Deng Alor alisema bila ya kundi hili migawanyiko ya kisiasa katika serikali ya Juba ambayo ilisababisha mapigano kuendelea basi hakutakuwa na amani. " tatizo lilianza ndani ya mfumo wa kisiasa, lilianza na sisi kundi la tatu. Tunatofautiana juu ya masuala ya mageuzi na demokrasia katika chama. Tulisisitiza juu ya mageuzi. Kama unataka kutatua mzozo huu unatakiwa kusuluhisha tofauti ndani ya chama tawala".

Baada ya zaidi ya miezi mitatu ya mapigano mafanikio pekee ya utaratibu wa amani yaliyopatikana ni sitisho la mapigano ambalo limekuwa likikiukwa mara kwa mara tangu mwezi Januari.
Wanadiplomasia wa kimataifa wanaishiwa na ustahmilivu na wiki hii waliwaonya wadau wote huko kutakuwa na madhara kwa wale ambao wanavuruga maendeleo. Alisema mwakilishi maalumu wa Marekani kwa Sudan Kusini, Donald Booth. "Kama serikali au mtu mwingine yeyote anajaribu kudumaza utaratibu wa amani na kuwakejeli viongozi wa nchi wanachama wa IGAD, watakabiliwa na madhara. Watu wa Sudan Kusini wanatarajia kufanyika tena kwa mashauriano. Wanatarajia sauti zao zitasikika katika kusukuma mbele amani endelevu. Biashara kama kawaida siyo njia muafaka ya kusonga mbele".
Jenerali Taban Deng Gai anaongoza mashauriano kwa upande wa upinzani unaomtii Makamu Rais wa zamani, Riek Machar. Anasema kwamba kinyume na serikali ya Rais Salva Kiir wao wapo tayari kwa mazungumzo na wahusika wote.
Voaswahili (R.M)

No comments:

Post a Comment