MAN U YAPANGWA NA BAYERN,CHELSEA NA PSG
Manchester United imepangwa kucheza na
Bayern Munich katika michuano ya robo fainali ya ligi ya mabingwa
barani Ulaya huku Chelsea ikipangwa kukutana na Paris St-Germain.
Mabingwa wa ligi ya Uhispania,
Barcelona watapambana na Atletico Madrid, huku Real Madrid ikipangwa
kukutana na Borussia Dortmund.
Mechi zao za mzunguko wa kwanza zitaanza tarehe 1 mpaka 2 mwezi Aprili na marudiano yatakuwa tarehe 8-9 Aprili.
Fainali ya michuano hiyo itachezwa katika uwanja jijini Lisbon wa Estadio da Luz tarehe 24 mwezi Mei.
Manchester na Bayern wanakutana tena
tangu mwaka 1999 kwenye fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa, ambapo
Ole Gunnar Solkjaer na Teddy Sheringham waliiwezesha Manchester kutwaa
kikombe chini ya Kocha wao Alex Ferguson.
Mara baada ya kupangwa kwa timu hizo nchini Switzerland, kiungo mshambuliaji wa Bayern, Philipp Lahm amesema kuwa hawawezi kutetereshwa na nafasi waliyonayo United kwa sasa katika ligi kuu na kusema kuwa watasafiri mpaka Manchester kwa kazi moja tu, nayo ni kufunga magoli.
Chelsea inayoongoza kwenye msimamo wa ligi itaifuata PSG nchini Ufaransa katika mzunguko wa kwanza.
bbcswahili (R.M)
No comments:
Post a Comment