RAIS WA IRAN AANZA SAFARI YA KUTEMBELEA OMAN
raisi wa Iran, Hassan Rouhani
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran leo ameanza safari yake ya siku mbili ya kuitembela
nchi ya Oman. Kabla ya kuelekea Oman Rouhani amesema kuwa, lengo la
safari yake hiyo ni kuimarisha uhusiano wa pande mbili na kujadili
masuala muhimu zaidi ya kieneo na kimataifa.
Dakta Rouhani ameeleza kuwa, safari
hiyo inafanyika kwa mwaliko uliotolewa na Sultani Qaboos wa Oman na
kwamba siku zote kuimarishwa uhusiano wa pande zote na nchi za Kiislamu
hasa zilizo jirani ni muhimu kwa Jamhuri ya Kiislamu.
Dk. Rouhani pia amesema ana matumaini
safari yake hiyo nchini Oman itakuwa na matokeo mazuri katika kuimarisha
amani na usalama wa kudumu katika eneo la Ghuba ya Uajemi. Hii ni mara
ya kwanza kwa Rais Hassan Rouhani wa Iran kuitemblea moja ya nchi za
Kiarabu za Ghuba ya Uajemi tangu aingie madarakani mwezi Agosti mwaka
jana.
Chanzo, tehranswahili.com (R.M)
No comments:
Post a Comment